Na. Mwandishi wetu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip…
Mwenyekiti wa jumuiya ya CCM ya Umoja wa wazazi mkoa wa Kigoma Dr. Nicholaus Zacharia amezuru na kukagua mradi wa kitegauchumi cha chama cha mapinduzi wilaya ya Kibondo baada ya kuombwa na mwenyekiti wa CCM wilayani humo
Ziara hiyo ya kushitukiza imefanyika jana wakatii mwenyekiti wa wazazi akitokea mkoani Kagera kuhani msiba wa mama wa Katibu wa Wazazi wilaya ya Buhigwe aliyefariki wiki iliyopita
Akizuru mradi wa maduka na kituo cha burudani kinachojengwa mkabara la makao makuu ya CCM wilaya ya Kibondo, Dr. Zacharia amepongeza uongozi wa chama wilayani humo kwa kuwa wabunifu na kutoa ushauri kwa wilaya nyingine kamatii za siasa zibuni miradi ya kukitegemeza chama.

Dr. Zacharia amesema, chama kinatakiwa kuwa na miradii ya maendeleo ambayo itatumika katika kuongeza mapato na kukiwezesha pia kumudu gharama za uendeshaji wa majukumu ya chama na kuwatumikia wanachama na kuisimamia serikali
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibondo Bw. Hamis Tahiro amemweleza mwenyekitii wa Wazazi kuwa kamatii ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Kibondo imejiwekeza utaratibu wa kubuni miradii mipya na kuendeleza miradi ya zamani ili kukipa mapatoo chama na kuiwezesha ofisi ya wilaya hiyo kujitegemea

Naye katibu wa CCM wilaya ya Kibondo Bw. Raphael Sumaye pamoja nakumshukuru Dr. Zacharia kukubali kutembelea mradi wa CCM wilaya ya Kibondo nje ya ratiba, amemtaja kama kiongozi mahili na mshauri mzuri katika masuala ya ujenzii wa chama na kujitegemea
Sumaye amemuomba mwenyekiti wa wazazi kuwa balozi wao kwa wadau wa maendeleo ili waendelee kukiunga mkono chama cha mapinduzi katika jitihada zake za kuwaletea maendeleo wanachama wake na watanzania kwa ujumla.