skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Prosper Kwigize- Njombe

Kama ilivyo desturi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuwasha na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka, Mwaka huu mwenge huo ambao ni alama muhimu kwa taifa la tanzania unawashwa mjini Njombe na kukimbizwa katika halmashauri izote nchini kabla ya kilele chake kitakachofanyika mkoani Kagera

Kwa mujibu wa kamatii ya maandalizi, shughuli zote za uandaaji zimekamilika na sherehe hizoo ambazo ni kivutio kwa watanzania na mataifa mbalimbali duniani zitafanyika katika uwanja wa Sabasaba ambapo mgeni rasmi atakuwa makamu wa rais wa Tanzania Dr. Philp Mpango

Katika maadhimisho hayo yanayobeba ujumbe mahususi kwa kila mwananchi, kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwahimiza wananchi kujitokeza katika sensa ya watu na makazi kama nguzo mhimu ya maendeleo pamoja na Kuzuia rushwa, kuhimiza Lishe bora, kutokomeza malaria, pamoja na kuzingatia usawa katika mapambano dhidii ya virusi vya ukimwi.

Aidha mwenge wa Uhuru mwaka 2022 ni sehemu ya mikakati ya kitaifa ya kupambana na madawa ya kulevya ambayo kwa sehemu kubwa yamekuwa na mchango ya kuharibu nguvu kazi ya vijana na kuzorotesha maendeleoo ya kundi hilo mhimu kwa taifa.

Mawaziri mbalimbali akiwemo Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia masuala la Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu, ambaye ni mwenyeji wa sherehe hizo akishirikiana na waziri wa habari, vijana, utamaduni na Michezo wa Zanzibar.

Ujumbe mahususi wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2022

Wananchi kote nchini wanapewa shime kuhudhuria shamrashamra za mbio hizo sambamba na kusikiliza ujumbe mahususii wa mwenge utakaotolewa na vijana sita walioteuliwa kumwakilisha rais Samia Suluhu Hassan kuukimbizi mwenge huo nchi nzima.

Wakimbiza mwenge mwaka huu ni Rodrick Romward Ndyamkama kutoka Mwanza, Sahili Nyanzabara Gararuma kutoka Njombe, Zadida Abdalla Rashid kutoka Kusini Pemba, Grolia Festo Peter kutoka Singida, Ali Juma Ali kutoka Mjini Magharibi na Emanuel Ndege Chacha kutoka mkoani Kagera.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma