WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua jengo la wagonjwa wa dharura kwenye hospitali ya wilaya ya…
Matinde Nestory -Mwanza
Wavuvi wa samaki na dagaa katika ziwa Victoria wameshauriwa kuachana na uvuvi haramu ili kuepuka kuua mazalia ya samaki na dagaa katika ziwa hilo ambalo ni tegemeoo la kitoweo cha samaki adimu duniani.
Rai hiyo imetolewa Mei 16 mwaka huu na waziri wa mifugo na uvuvi Mashauri Mashimba Ndaki wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa uvuvi kutoka Kanda ya ziwa mkoani Mwanza na kueleza kuwa uvuvi haramu unasababisha samaki kupotea katika ziwa Hilo.
Waziri Ndaki amesema kuwa hakuna watu wengine wanaoweza kukomesha uvuvi haramu tofauti na wavuvi wenyewe, wauzaji nyavu, wasimamizi pamoja na viwanda vinavyochakata samaki.
“Ni lazima tushirikiane kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa katika ziwa Victoria unaoendelea kwa Sasa haiwezekani tunakosa samaki kwa sababu ya watu wachache ambao hawafati masharti ya uvuvi” Amesema Waziri Ndaki.
Amesema kuwa vitendo vya uvuvi haramu vimekithiri katika ziwa hilo, hivyo serikali itahakikisha unatumia Sheria kuthibiti uvuvi haramu.
“Tutatumia nguvu kuthibiti uvuvi haramu, serikali ipo tunajua wanaohusika ni wavuvi wenyewe, wasambazaji wa nyavu zisizo halali, tutashughulika na wale wanaovua samaki wadogo kila kitu kitakamatwa iwe gari iliyobeba samaki, boti, Godown tutakamata, viwanda wanavyochukua samaki wadogo wadogo tutakamata” Amesema Waziri Ndaki.
Nae mmoja wa wadau wa uvuvi Charles Tizeba amesema kuwa sheria iangaliwe ili ili kufanya marekebisho ya vifungu vyenye mkanganyiko, ili kupunguza uvuvi haramu, kodi ifanane katika halmashauri zote