skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Shirika linalotoa huduma za afya kwa wakimbizi na wenyeji katika mkoa wa Kigoma linalofahamika kwa jina la Medical teams International limetoa mmisaada yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2 kusaidia uimarishaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini Tanzania ikiwemo kwa wakimbizi na wenyeji mkoani Kigoma

Akitoa Taarifa kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu aliyewakilishwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa polisi Thobias Andengenye ambaye amezuru katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na baadaye kuzindua ujenzi wa jengoo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi mkazi wa Medical Teams Internation (MTI) Dr. George Mwita, amebainisha kuwa misaada iliyotolewa ni pamoja na vifaa tiba, madawa na ujuzi wa watoa huduma ngazi ya jamii

Dr. Mwita amebainisha kuwa MTI inalenga kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania na jumuiya za kimataifa kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kutekeleza afua mbalimbali za afya ya uzazi hasa kwa mama na mtoto ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi za kiafya.

Dr. George Mwita, Mkurugenzi wa shirika la Medical Teams International nchini Tanzania

Amesisitiza kuwa katika kutimiza dira hiyo shirika la Medical teams limeokoa zaidi ya akina mama wajawazito 4237 kwa kuwawezesha kujifungua salama bila kupata kifoo cha mjamzitoo hata mmoja katika vituo ambavyo shirika hilo linasaidiana na serikali kutoa huduma.

Mwita ameweka bayana kuwa mkoa wa Kigoma ni mnufaika mkuu wa huduma na misaada ya kiafya inayotolewa na wahisani na kwamba kupitia katika shirika la MTI, Kigoma imepata misaada ya vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya hospitali mbalimbali za kijamii pamoja na vituo vya kutoa huduma kwa wakimbizi katika wilaya za Kakonko, Kasulu, Kibondo, na Kigoma

Kwa upande wake Waziri Ummy Mwalimu kupitia kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma amepongeza na kushukuru shirika la Medical Teams International kwa kukubali kushirikiana na serikali kutatua changamoto mbalimbali za kiafya hususani uchangiaji wa vifaa tiba, ujenzi wa majengo ya kutolewa huduma za matibabu na kuwajengea uwezo watumishi wa serikali na watoa huduma ngazii ya jamii.

Shirika la Medical teams International linashirikiana na Chama cha Msalaba mwekundu kutoa huduma za afya na matibabu kwa wakimbizi katika kambi zaNduta na Nyarugusu mkoani Kigoma.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma