skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Joel Daud na Evarist Kitungwa…

Wananchi wa mkoa wa Kigoma wameshauriwa kujijengea utamaduni wa kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa vishale maarufu kama Darts ili kuimarisha utimamu wa miili yao Pamoja na afya ya akili ndani ya jamii zao.

Wito huo umetolewa hii leo na mwezeshaji wa mafunzo kwa waandishi wa Habari Bwana Prosper Kwigize  wakati wa uzinduzi wa mchezo wa vishale uliofanyika katika viwanja vya Buha Radio vilivyopo wilaya ya kasulu mkoa wa Kigoma ulioendasambamba na uzinduzi wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa Habari . Bwana Kwigize Amesema kuwa mchezo huo umekuwa na mchango mkubwa katika kumjenga mtu kiakili anayeshiriki kwa kuwa unamfanya mchezaji  kufikiri Zaidi kimahesabu namna ya kucheza  mchezo huo ili aweze kuwa mshindi dhidi ya washindani wenzake.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki waliohudhulia katika uzinduzi huo wameelezea kufurahishwa na mchezo huo kutokana na umuhimu wake kwa afya ya wanamichezo. Naye mshindi wa mchezo huo wa vishale Bwana Mussa Mkilanya ameelezea namna alivyoshiriki na kuibuka mshindi  katika siku ya kwanza ya uzinduzi wake .

Mshindi wa shindano la Vishale mafunzoni Bw. Mussa Mkilanya, Buha FM iliutumia mchezo huo kukomaza ubongo

Licha ya mchezo huu kuwa Rafiki kwa afya ya mchezaji bado suala la michezo hii imekuwa haipewi nafasi kubwa na watanzania wenyewe  hali inayopelekea  mchezozo huo kuwa na ushiriki wa watu wachache ikilinganishwa na mingine hapa mchambuzi wa masuala ya michezo John Eliasi amesema wachezaji wengi wanatazamia mpira nakuwataka kupokea fursa ya mchezo wa vishale kwa kuwa ni njia pekee ya kufanikiwa kutokana na kutokuwepo kwa washiriki wengi.

Bw. Optatus Likwelile Kiongozi wa OHIDE akicheza mchezi wa Vishale kuhamasisha washiriki wa mafunzo

Uzinduzi wa mchezo wa vishale umezinduliwa Rasmi hii leo tarehe 24 oktoba,2021 na tamati yake itakuwa tarehe 26 oktoba,2021 na  kuhudhuliwa  na washiriki takribani tisa wakiwemo wenyeji wa wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma na wengine kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma