skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Joel Daud, Muleba- Kagera

Wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Muleba mkoani kagera wametakiwa kusoma kwa bidii wakati wote ili kutimiza ndoto zao kupitia elimu na kuondokana na tabia mbaya zinazopelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo yao kwa kujihusisha na makundi yasiyofaa wawapo shuleni

Wito huo ulitolewa na mbunge wa jimbo la Muleba kusini mhe.  Daktari Oscar Inshengoma Kikoyo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya IBN Hambal Islamic sekondari iliyopo wilayani Muleba  baada ya kukabidhi zawadi ya mifuko miamoja 100 ya saruji  yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kama ahadi aliyoitoa hapo julai mwaka jana 2021 baada ya kutokea janga la moto lililounguza bweni la wasichana shuleni hapo.

Shehena ya Saruji iliyotolewa na Mhe. Ishengoma kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari

Mhe. Kikoyo alisema licha ya miundombinu kuendelea kuwa bora kwa shule mbalimbali wilayani Muleba bado kuna umuhimu kwa wanafunzi kutenga muda wa kutosha wa kusoma wawapo shuleni hali itakayowasaidia kufaulu masomo yao vizuri ili kuukabili ushindani mkubwa uliopo kwa sasa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Wanafunzi lazima mujiandae ipasavyo kuwa na nidhamu kitu cha kwanza kitu cha pili mfaulu masomo yenu na kingine kujiamini kwa hiyo maisha yenu ya mbele yatakuwa mazuri sana na sisi wengine tunachangia na ndiyo maana tuko hapa mlipopata ajali ya moto usiku nilikuja hapa na nikatoa ahadi na ndiyo maana leo nimekuja kutimiza ile ahadi niliyoitoa ya kuchangia mifuko miamoja ya saruji ili mkasome vizuri”.Alisema

Pia, katika hatua nyingine mhe. Oscar Kikoyo aliwakumbusha wanafunzi wote wilayani Muleba pindi watakapokwenda likizo fupi kupisha zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika hapo mwezi August mwaka huu wa 2022 kwenda kuhamasisha jamii kuhesabiwa .

“Tunakwenda kwenye Sensa ya watu na makazi mtakuwa likizo tunawaomba mtakapokuwa likizo wahamasisheni wazazi na walezi wenu wakahesabiwe tunapohesabiwa ndipo tutajua hapa Muleba tunahitaji Barabara serikali inatumia hizo takwimu kupanga mipango ya maendeleo”.Alisema

kwa upande wake mkuu wa shule ya IBN Hambal Islamic secondary Ayoub Suleiman Hamis alitoa shukurani za dhati kwa niaba ya shule kwa mhe. mbunge wa jimbo la Muleba kusini Dakta.Oscar Inshengoma Kikoyo kwa kutoa mifuko miamoja ya Saruji  kwa ajili ya ujenzi wa bweni jipya la wasichana wa shule hiyo…

Mhe.mbunge amefikisha mifuko 100 ya Saruji kwa kweli tunamshukuru sana hatuna cha kumlipa isipokuwa mwenyezi Mungu atamlipa bweni lilikuwa linabeba wanafunzi 103 tulipotathimini tuliona kwamba kulikarabati linakuwa na gharama kubwa tukaanzisha msingi mpya hivyo tunajenga bweni jingine jipya. Fedha inayohitajika ni milioni 60 mpaka bweni kukamilika  lakini tayari wadau wengine wamechangia Halmashauri ilitoa mabati mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wamechangia hivyo; kwa mifuko hii ya mbunge tutakuwa tunapungukiwa milioni 20 hadi bweni kukamilika”.Alisema Suleimani

Nao baadhi ya wanafunzi wasichana waliouguliwa na bweni lao akiwemo Hasira Suleimani na Salima Iburahimu walitoa shukurani zao kwa niaba ya wanafunzi wa IBN Hambal Islamic Secondary kwa kupokea Saruji hiyo kutoka kwa mbunge wao ili  kukamilisha ujenzi kwa kuwa kwa sasa wamekuwa wakilala msikitini na kueleza kukamilika kwa bweni kutawaondolea changamoto kubwa waliyoipitia kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuungua kwa bweni lao Julai 23 mwaka 2021.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma