skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane na Prosper Kwigize – Kigoma

Zaidi ya raia 2600 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameingia nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi kufuatia machafuko yanayoendelea katika mikoa ya mashariki

Akizungumzia hilo mratibu wa Kanda ya Idara ya Huduma ya Wakimbizi Nashon Makundi alisema zoezi la kuwatambua waomba hifadhi hao lilianza rasmi Machi 05 na kwamba walianza kuingia nchini kinyume na taratibu toka mwezi Septemba 2022 mpaka January 2022.

“Asilimia ndogo ya waomba hifadhi wanaingia nchini kutokea Kongo moja kwa moja huku wengi wao wakiwa wamekwishaingia nchini muda mrefu bila kufuata taratibu kwa madai kwamba hawakuwa na taarifa sahihi za kuomba hifadhi wakidhani kwamba nchi imefunga mipaka ya kuwapokea waomba hifadhi ila  baada ya kujua mipaka ya nchi ipo wazi wameanza  kujitokeza kila walipo kuja kuomba hifadhi”Alisema Makundi.

Makundi alisema idadi yao iliongezeka zaidi kuanzia Ijumaa Machi 10 ambapo walianza kupokea watu kati ya 300-600 kwa siku na mpaka sasa wameshapeleka watu 630 katika kambi ya Nyarugusu waliokwisha kuhojiwa kwaajili ya zoezi la kuomba hifadhi huku mchakato wa kuwatambua na kuwasajili ukiendelea na kwa watakaokidhi vigezo vya kuwa wakimbizi watapewa hadhi hiyo.

Maafisa wa mshirika ya kiutu wakitoa misaada ya awali ya chakula kwa wakimbizi wapya kutoka DRC

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewaasa wananchi wa mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kufuata sheria inayowakataza kutopokea watu wanaoingia nchini bila kupia kwenye mipaka halali na kuwataka waomba hifadhi  kuwa watulivu wakati suala lao litakaposhughulikiwa na maafisa na kwamba watoe taarifa za kweli kwani ndizo zitakazoamu hadhi yao.

Usiingie kwenye nchi ya watu na kuomba hifadhi kwa watu bila kupita serikalini na kufuata sheria, ni lazima tujifunze kufuata sheria kokote na mahali popote unapokwenda na yanapotokea machafuko katika nchi zao lazima wajisalimishe kwenye serikali ili wawatambue na kuwasaidia kwaajili ya usalama wa anayekupokea, wa kwako na wa nchi kwa ujumla” alisisitiza Mkuu wa mkoa wa Kigoma.

Mratibu wa wakimbizi kanda ya magharibi inayohusisha mkoa wa Kigoma Bw. Nashon Makundi amebainisha kuwa kundi hilo linahusisha wakimbizi wapya walioingia moja kwa moja kutoka DRC pamoja na waliokuwa wakiishi nchini kwa siri bila vibali ambao wamejitokeza kufuatia kuwepo kwa wimbi hilo jipya la raia wenzao kuvuka mpaka.

Waomba hifadhi hao wanaoundwa na kundi kubwa la wanawake na Watoto wameiambia CA kuwa kinachowakimbiza na kuiacha nchi yao ya DRC ni ongezeko la mashambulizi ya M23 wanaokabiliana na majeshi ya serikali ya DRC kunakosababisha mauaji ya raia katika eneo la Kivu kaskazini na Kivu kusini hususani eneo la Goma.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini Sudi Mwakibasi alisema wanatekeleza jukumu la msingi la kuwahifadhi waomba hifadhi na wakimbizi saw ana mkataba wa Geneva Formation wa mwaka 1951 na itifaki ya mwaka 1967 ya kuwapokea waomba hifadhi kutoka nchi yoyote duniani.

Sikiliza hapa ripoti ya mwandishi wetu Prosper Kwigize aliyehudhuria eneo linalopokea wakimbizi hao mjini kigoma kwa maelezo zaidi

Waomba hifadhi wengi ambao ni wanawake na watoto wametoka eneo Kivu kaskazini na Kusini hususani eneo la Goma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma