Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais…
Mabalozi kutoka nchi tano za Umoja wa Ulaya pamoja na Uingereza leo wameanza Ziara katika mkoani wa Kigoma magharibi mwa Tanzania kwa ajili ya kushududia shughuli za kuhudumia wakimbizi
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR, mabalozi hao watatembelea kambi za wakimbizi wa Mtendeli wilayani Kakonko, Nduta wilayani Kibondo na Nyarugusu wilayani Kasulu.
Mabalozi hao ni pamoja na
1. H.E Peter VAN ACKER: Balozi wa Belgium
2. H.E Mette Norgaard DISSING-SPANDET: Balozi wa Denmark
3. H.E. Regine HESS: Ambassador, Balozi wa Germany
4. H.E Jeroen VERHEUL – Balozi wa Netherlands.
5. H.E David CONCAR – Balozi wa Uingereza.
6. H.E Didier CHASSOT – Balozi wa Uswiss
Matumaini ya wakimbizi kwa ziara hiyo ni hatima ya ukimbizi wao na fursa za kwenda nchi ya tatu, huku wengine walilalamikia juu ya mpango wa kufunga kambi ya mtendeli na baadaye nduta mwaka huu.