skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Adela Madyane – Kigoma

Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) limeanzisha jimbo jipya nichii Tanzania sambamba na kumsimika rasmi askofuu mpya wa jimboo la Magharibi Kigoma, ambaye anaanza kazi rasmii baada ya kuwekwa wakfu na viongozi wa kanisa hilo.

Akihubiri katika ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa askofu mteule wa jimbo jipya la Kigoma, Askofu mkuu wa kanisa hilo Fredrick Shoo, amewapongeza waumini wa misioni ya Kigoma kwa kupanda daraja na kuwa jimbo baada ya kipindi kirefu tangu kanisa la KKKT lilipoingia mkoani Kigoma miaka ya 1980.

Aidha Shoo ametoa witoo wa mshikamano kwa waumini na viongozi wote wa kanisa hilo katika kumtumikia Mungu.

Kwa upande wa Askofu Jackson Mushendwa aliyewekwa wakfu kuwa askofu mkuu wa dayosisi ya Magharibi akisaidiwa na Melikizedeki Kusesa amesema kama dayosisi mpya washirika wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanasimama kwa miguu yao wenyewe

“Tijidhatiti kufanya kazi ili kukidhi mahitaji yetu yote muhimu ya chakula, mavazi, elimu , afya na malazi bila na kunung’unika, wala kutegemea watu wengine, tuhimizane kufanya kazi hasa vijana ambao wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii badala ya kufanya kazi”amesema askofu Mushendwa

Wakati, huo huo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) askofu Fredick Shoo ametoa wito kwa wananchi kutunza mazingira ili kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi.

Ameyasema hayo wakati wa sherehe za uzinduzi wa dayosisi ya Magharibi mkoani Kigoma baada ya kanisa hilo kudumu kuwa mission kwa muda wa miaka 40 toka mwaka 1982, na kuifanya kuwa dayosisi ya 27 pamoja na kumsimika askofu mkuu wa dayosisi hiyo.

Amesema kumekuwa na ongezeko la joto kote duniani litokanalo na athari za uharibifu wa mazingira hivyo ni lazima kuhakikisha elimu ya utunzaji wa mazingira inatolewa kwa rika zote ili kukabiliana na hali iliyopo

“Joto limeongezeka kote duniani, majira tuliyoyatarajia na mpangilio wake vimeharibika kabisa, ni muhimu kwa wananchi kushirikiana na serikali kukabiliana na changamoto hizo kwa pamoja” alisema askofu Shoo

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma