skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Takribani shilingi Milion 36.7 zimepatikana kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa vituo vya afya vipya 7 ambavyo vinajengwa katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.

Akiongoza harambee hiyo  leo Mufti na Sheikhe Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuberi bin Ally katika viwanja vya Nyamagana vilivyopo jijini Mwanza.

Mufti Zuberi amesema kuwa fedha taslim pamoja na ahadi ya fedha ambayo ni shilingi milioni 102,69,000 ambapo jumla ya fedha hizo taslim na ahadi  zimepatikana ni shilingi milioni 139,445,900 ambazo zitatumika kujenga vituo hivyo.

“Tunataka tuwe na hospital ambazo akina mama watakuwa wanatibiwa na akina mama wenzao ni neema kubwa tukiziona hospital za namna hii,miaka nenda rudi hakuna lakini tutazipata kwa harambee Kama hizi”amesema Mufti Zuberi.

Aidha amesema kuwa fedha hizo zimetolewa na viongozi mbalimbali wa kiserikali,viongozi wa madhehebu mbalimbali,taasisi,MaSheikhe kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na wananchi kwa ujumla.

Hata hivyo amewataka Waislam kujitoa na kujitolea katika kuchangia ujenzi wa vituo hivyo ili visaidie jamii Kupata huduma ya afya.

Nae Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza Salum Kali amesema kuwa vituo vya Afya vipya vitaisaidia serikali na jamii kwa ujumla Kupata huduma ya Matibabu pamoja na  kupatikana kwa ajira.

“Sisi wananchi wa Mkoa wa Mwanza tunaunga mkono Harambee hii ndio maana tuko hapa kuhakikisha Jambo hili uliolionesha linafanikiwa”amesema kaimu Mkuu wa Mkoa Kali.

Kwa upande wake katibu Mkuu  wa Baraza la Waislam Tanzania Mkoa wa Mwanza Ramadhani Chanila ambaye amesoma risala amesema kuwa BAKWATA imeamua kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhudumia jamii bila kujali itikadi ya dini pamoja na kusogeza huduma ya afya kwa wananchi. 

“Tumeanza mradi huu na huku tukizingatia mikakati wa miaka mitano katika awamu hii ya kwanza tumeanza na majengo ya nje OPD hii ni kwa wilaya zote Saba ambapo majengo yote yatagharim kiasi Cha shilingi Bilion 2,416,182,825″amesema Chanila.

Ameongeza kuwa jengo la OPD litaambatana na ujenzi wa mfumo wa maji safi,choo Cha nje,shimo la taka, ujenzi wa kichomeo taka pamoja na ujenzi wa choo Cha watu wenye mahitaji maalum.

Nao baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wamesema kuwa harambee hii imekuwa na mafanikio na kuwaomba watu wenye uwezo kujitolea mchango wa ujenzi wa vituo vya afya mchango huo ambao utasaidia jamii Kupata huduma ya afya kwa ukaribu.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma