skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Tanzania leo imepata makamu war ais mpya baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteuwa Waziri wa Fedha na Mipango kuwa makamu wake na kisha kuthibitishwa na bunge kwa kura 363 sawa na asilimia 100 ya wabunge wote waliohudhuria mkutano huo.

Katika hali ya kushtusha wengi, leo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kushauliana na kamati kuu ya chama cha mapinduzi katika kikao maalumu, anawasilisha jina la Waziri wa fedha Philip Mpango kuwa makamu wake.

Jina hilo limewasilishwa na mpambe wa Rais maarufu Mlinzi, ambaye majira ya saa nne asubuhi saa moja tu baada ya kikao cha Bunge kuanza kujadili mipango ya maendeleoo katika bajeti ya waka 2021-2022, na Spika wa bunge anafungua bahasha na kukuta uteuzi wa Waziri Mpango na kuwatangazia wabunge ambao hata kabla ya kulipigia kura jina hilo wanaibua vigeregere na bashasha wakiunga mkono uteuzi huo.

Akiongea kabla ya kupigiwa kura hizo mheshimiwa Makamu wa Rais mteule Dr. Philip Mpango ameahidi kuwa atafanya kazi kwa bidii na hasa kuhakikisha anasimamia utekelezaji wa miradi yote iliyoasisiwa na hayati Dr. John Pombe magufuli ikiwemo miradi mikubwa ya miundombinu ya umeme, barabara, maji na afya.

Aidha Mpango ameahidi kumsaidia Rais Samia kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma sambamba na kutokomeza Rushwa kama sehemu ya kuwahudumia wananchi wanyonge na masikini.

“Mimi siyo mpole kama mlivyonisifia, mie ni mkali hasa pale ninapoona kuna ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha za umma” alisisitiza Dr. Mpango akilihutubia Bunge kabla ya kuaga na kuanchia ngazi hiyo ya uwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.

Baada ya uwasilishaji wa jina hilo, bunge likawa na wajibu maalumu wa kupiga kura ya ndiyo ama hapana, ambapo wabunge waliohudhuria kikao hicho walikuwa 363 na wote wakapiga kura ya ndiyo kuunga mkoano uteuzi huo

Kwa upande wake viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Kigoma anakotoka Dr. Mpango ambaye alikuwa mbunge wa jimbo la Buhigwe, wamepongeza sana uteuzii wa mbunge wao kuwa makamu wa Rais. Kajoro Vyohoroka ni Katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kigoma, yeye anabainisha kuwa Mkoa wa Kigoma na chama cha mapinduzi wanajivunia kwa kumteua na kisha kumpigia kura Dr. Mpango na kwamba kitendo cha kuteuliwa kuwa makamu wa Rais ni uthibitisho tosha kwamba ni kiongozi anayefaa. Kajoro amesisitiza kuwa, Tanzania imepata viongozi bora wenye maono mapana na uchungu wa maendeleo.

Wananchi wa kawaida mkoani Kigoma nao licha ya kutoamini kilichotangazwa, wameshikwa na bashasha kubwa na wengi wao wameonesha matumaini juu ya uteuzi wa Dr. Mpango. Genoveva muhini ni mmooja wa wananchi wa Kigoma waliokutwa wakisali na kushukuru kwa uteuzi huo. Anasema giza lililokuwa limetanda miongoni mwa watanzania limeisha na kwamba wanaimani na Mpango kutokana na historia yake ya utendaji.

Watanzania wengi walikuwa na mashaka kuwa huenda ndoto za aliyekuwa Rais hayati magufuli zitakwama hususani miradi mikubwa ya kimkakati, hata hivyo Dr. Mpango amekiri kuwa serikali bado inawajibu wa kutekeleza miradi yote, jambo hili linamwibua Masoud Bigangika mkazi wa Kasulu magharibi mwa Tanzania ambaye anakirii kuwa kuteuliwa kwa Dr. Mpango ni mwarobaini tosha wa kutekeleza miradi yote ya kimkakati ikiwemo kudhibiti matumizi yasiyofaa na ufisadi..

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kurugenzi ya habari Ikulu mjini Dodoma, halfla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Dr. Philip Isidory Mpango zitafanyika kesho Ikulu ya Chamwino Dodoma

Prosper Kwigize

Kigoma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma