skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Dodoma

Tanzania imeripoti kuendelea kuwepo kwa maambukizi na wagonjwa wa homa ya UVIKO 19, huku ikitangaza kuwepo kwa visa vipya 442 vya watu waliopata maambukizi mapya katika kipindi cha Oktoba na Decemba mwaka huu

Akitoa taarifa hiyo leo mchana, Mganga mkuu wa serikali Dkt. Tumaini Nagu amebainisha kuwa idadi hiyo ya maambukizi ni kubwa mno ukiringanisha na watu 272 waliopata maambukizi katika kipindi kilichotangulia

Dkt Nagu amebainisha kuwa kiwango hicho cha maambukizi ni saw ana asilimia 62.5 na kwamba hakuna mgonjwa aliyelazwa hospitalini na hakuna kifo kilichoripotiwa.

Wakatii huo huo jumla ya watanzania milioni 29 kati ya milioni 30 wamepatiwa chanjo ya UVIKO 19 tangu kuanza kwa utoaji wa chanjo hiyo mwaka 2021.

Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa witoo kwa raia wake kupata chanjo ili kuepuja madhara Zaidi yanayotokana na maambukizi ya virusi vya Corona vilivyosambaa duniani tangu mwaka 2020.

Idara ya afya nchini Tanzania inawataka watu wote wanaohisi kuwa na dalili ya maambukizi kuhakikisha wanavaa barakoa muda wote, watu wote kumilisha dozi za chanjo na kuendelea kujikinga kwa kunawa mikono kila mara kwa majii safi au vitakasa mikono (sanitizer).

Serikali ya Tanzania inatoa wito kwa watu wote wenye dalili za magonjwa ya mfumo wa hewa, Homa, Mafua, kikohozi, maumivu ya viungo, vidonda vya koo na kuumwa kichwa Kwenda katika vituo vya afya ili kupatiwa matibabu stahiki.

Kwa sasa nchi ya China ndiyo inayoripoti visa vingi vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona duniani.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma