skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mkurugenzi wa huduma za usimamizi bodi ya Pamba Tanzania James Shimbe  amewaomba wananchi na wakulima kujifunza namna ya kulima Kilimo bora  Cha Pamba kwa kuzingatia kanuni za Kilimo na Kupata uzalishaji wenye tija.

Rai hiyo imetolewa Leo na mkurugenzi huyo katika maonesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo vilivyopo wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

James amesema kuwa wakulima wametakiwa kujifunza kanuni bora za Kilimo kwa kufuata taratibu na kanuni hii itasaidia Kupata uzalishaji mkubwa katika eneo dogo.

“Sisi tupo kwa ajili ya kuwaonesha wakulima namna Pamba inavyozalishwa kuanzia mwanzo mpaka kuichakata kwenye viwanda Kupata nyuzi na hatimaye kufikia hatua ya mwisho ambapo tunapata mafuta ya kula”amesema Shimbe.

Mkurugenzi wa huduma za usimamizi bodi ya pamba Tanzania James Shimbe.

Akizungumzia changamoto amesema kuwa miaka ya karibuni wamekuwa wakipambana na viuadudu chawajani wamekuwa wakivamia mashamba na kuyaharibu ambapo wamekuwa wakishirikiana na watu wa utafiti kuweza kuwathibiti wadudu hao.

Ameongeza kuwa viuaduau 

wamesha sambaza kwa msimu wa 2021/2022 viuadudu Zaidi ya Milion 9 kukabiliana na wadudu hao wanaoleta usumbufu ambapo mwanzoni  hawakuwepo hii inatokana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha amesema kuwa malengo ni kuwafikia wakulima  Zaidi ya mikoa 17 ambayo ipo Sasa na kuendelea kufikia mingine yenye ardhi nzuri kwa Kilimo Cha pamba ambapo msimu uliopita ulikuwa  na Zaidi ya Tani 148,000 hii imetokana na kuchangia kwa elimu ambayo wakulima wamekuwa wakipewa.

“Kwa Sasa tumeleta mabadiliko tunapanda Miche 44,444 ni Mara mbili ya hapo awali ambapo uzalishaji unaongezeka Zaidi tofauti na hapo awali tulikuwa tunapanda Miche 22,222” amesema Shimbe.

Hata hivyo amesema kuwa ubora umeongezeka Kutokana na wakulima wamekuwa wakifuata kanuni bora za Kilimo na kuwataka kuendelea kujifunza kulima  Kilimo chenye tija.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma