Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Na. Matinde Nestory, Mwanza
Waumini wa dini ya kiislamu na wananchi wote kwa ujumla Mkoani Mwanza wameombwa kujitokeza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vituo vya Afya vipya saba (7) katika Mkoa wa Mwanza ili kupunguza uhaba wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Wito huo umetolewa Leo na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke wakati akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) ikiwa na lengo la kusaidia serikali katika kutoa huduma ya jamii.
Sheikhe Kabeke amesema kuwa waumini wa dini zote na wananchi kwa ujumla kujitokeza July 30 Mwaka huu katika viwanja vya Nyamagana kuchangia ujenzi wa vituo hivyo ambavyo vipo katika wilaya ya Ilemela, Nyamagana, Magu, Ukerewe, Misungwi, Kwimba na Sengerema.
“BAKWATA Mkoa wa Mwanza tunaomba kuwaarika dini zote kujitoa na kujitolea michango ya ujenzi wa vituo vya afya Saba katika Mkoa wa Mwanza nawaomba niwafahamishe kuwa tunapokea, sio pesa tu katika harambe hii, tunapokea mchanga, kokoto, nondo, saruji na chochote kile Cha ujenzi” amesema Kabeke.
Video hapa chini inaonesha viongozi wa BAKWATA mkoa wa Mwanza wakisisitija jambo hili, bonyeza HAPA utazame video
Aidha amesema kuwa vituo hivyo vya afya vitajengwa na nguvu ya Umma Waislam na wasio Waislam kwa ajili ya kuisaidia serikali kutoa huduma ya afya kwa jamii.
Hata hivyo katika harambee hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri Mkuu wa Tanzania Khasim Majaliwa.
Nae Sheikhe wa wilaya ya Nyamagana Sheikhe Othuman Ndaki amesema kuwa harambee hiyo ambayo itatengeneza historia katika jiji la Mwanza na nchi jirani kwa kuvuka malengo na kuwaelekeza waislam na wasio Waislam kutengeneza historia ya kujenga vituo vya afya.
Kwa upande wake Mstashari wa Sheikhe Mkuu wa Mkoa Alhaj Banyanga ambaye pia ni mfanyabiashara jijini Mwanza amesema kuwa anawaomba watu wa dini zote na wenye uwezo kujitoa katika kujenga vituo vya afya hali ambayo itasaidia vijana Kujipata ajira.
Hata hivyo amewaomba wananchi wote kujitokeza katika harambee hivyo ambayo itasaidia kuongeza vituo vya afya katika Mkoa wa Mwanza.